BEKI wa
Yanga, Vincent Bossou, ametamka hadharani licha ya kukubali kipigo cha mabai
2-1 kutoka kwa Mbeya City lakini hatamsahau mwamuzi wa kati wa mchezo huo, Rajab
Mrope kutokana na maamuzi yake kuwa tata.
Yanga ilipata
kipigo hicho kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu
Bara, juzi, ambapo beki huyo raia wa Togo anasema hajawahi kuona maamuzi kadhaa
yaliyofanywa na refa huyo.
“Tumefungwa
na tunakubali matokeo lakini sitasahau alichokifanya refa, alikuwa na makosa
mengi na maamuzi tata kibao ambayo yametugharimu kwa kiasi kikubwa.
“Sidhani
kama marefa wa namna hii wataweza kulikomboa soka la Tanzania ambalo linataka
kupiga hatua kutoka hapa lilipo kwa sababu hawajiamini na hata kuchezesha
kwenyewe inakuwa shida na hata kusimamia maamuzi yao,” alisema Bossou.
Katika
mchezo huo, mwamuzi alikubali bao la pili la Mbeya City lakini baada ya
kuzongwa na wachezaji wa Yanga waliodai haikuwa sahihi kwa kuwa faulo
iliyopigwa ilitekelezwa bila ruhusa ya mwamuzi, refa huyo akaamuru faulo
irudiwe, Mbeya City nao wakamzonga wakilalamika, akabadili maamuzi tena na
kukubali kuwa ni bao na mpira uwekwe kati.
Post a Comment