KATIKA hali isiyotarajiwa, kwenye mazoezi ya klabu ya Simba yaliyofanyika asubuhi ya jana (leo jumanne), kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, walijitokeza wafungwa wawili wakiwa wameongozana na askari wakitaka kumuona  Shiza Kichuya.
Simba ipo hapa Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Prisons utakaopigwa leo kwenye Dimba la Sokoine.
Tukio hilo lilitokea wakati Simba wakiendelea na mazoezi huku mageti ya uwanja huo yakiwa yamefungwa kuzuia mashabiki kuingia ndani, ndipo wakafika wafungwa hao na kuomba kuonana na Kichuya.
Wakati mazoezi yakiendelea, geti moja la uwanja huo lilifunguliwa na mmoja wa askari akaingia ndani na kuwaomba viongozi wa Simba wawaruhusu wafungwa hao kuingia na kumsalimia Kichuya pamoja na wachezaji wengine wa Simba.
Hata hivyo, viongozi wa Simba waliwaruhusu ambapo wafungwa hao waliingia wakiwa wamevalia sare na kukutana na kocha wa Simba Joseph Omog ambapo aliwaruhusu kumsalia Kichuya pamoja na wachezaji wengine.
Baada ya tukio hilo, wafungwa hao waliondoka uwanjani huku wakiwa na furaha tele, na wakiitakia timu hiyo ushindi mnono kwenye mchezo wa leo Jumatano jioni.

Post a Comment

 
Top