TIMU za Muheza United ya Tanga na Sifa Politan ya Dar es
Salaam, leo Jumamosi zinatarajiwa kufungua dimba la michuano ya Kombe la
Shirikisho (FA), mchezo utakaopigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Michuano ya msimu huu inazishirikisha timu 86 kutoka 64 za
msimu uliopita ambapo bingwa mtetezi ni Yanga. Timu 16 ni za Ligi Kuu Bara, 24
za Ligi Daraja la Kwanza, 24 za Daraja la Pili na timu 22 za mabingwa wa mikoa
ambapo michuano itakuwa ni ya mtoano na itaendeshwa kwa raundi tisa.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred
Lucas, amesema: “Kabla ya kuanza kwa mchezo wa ufunguzi, kutapigwa mechi ya
maveterani wa Coastal Union dhidi ya African Sports ambapo mchezo huo utaanza
saa 8:00 mchana.”
Post a Comment