Licha ya kwamba Mbao FC walikubali kichapo cha mabao 3-0, beki huyo alionyesha uwezo mkubwa kuwakabili washambuliaji wa Yanga na kusababisha kwenda mapumziko timu hizo zikiwa 0-0.
Baada ya dakika 90 kumalizika, Pliujm, licha ya kuwa na bashasha la ushindi mnono, alikunwa na kiwango cha Kwasi Asante na kuamua kumfuata kumnong’oneza kitu kwa dakika kadhaa.
“Tulikuwa tunazungumza mambo ya kawaida tu, ila niseme kama watanitaka wala sina tatizo, kwani kazi yangu ni mpira, niliwahi kukuambia tulipokutana pale kambini Lamada Hotel siku mbili kabla ya mchezo wenyewe hao mabingwa watetezi wakinifuata niko tayari,” alisema Kwasi.
“Kingine ni kwamba, yule kocha tunafahamiana tangu akifundisha soka nchini kwetu Ghana, tulikuwa tunakutana mara kadhaa akiwa na timu yake kwenye michezo ya Ligi Kuu.”
Mghana huyo amejiunga na Mbao FC ya mkoani Mwanza msimu huu, akitokea Mbabane Swallows ya Swaziland, huku ikiwa ni mara yake ya kwanza kucheza ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
Post a Comment