WAMEPANIA bwana. Ndivyo unavyoweza kusema kwa Simba, baada
ya kudumu kileleni kwa siku 83, sawa na saa 1,992 katika mzunguko wa kwanza wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba ilianza kwa ushindi wa mabao 3-1, katika mchezo uliochezwa Agosti 20 huu,
kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, imemaliza mzunguko wa kwanza kwa
kufikisha pointi 35.
Wekundu wa Msimbazi wamevunja rekodi ya misimu minne
kutokana na kutoongoza kwa muda mrefu katika msimamo wa ligi hiyo.
Lakini msimu huu wameweza kuongoza katika mzunguko wa
kwanza, ambao misimu iliyopita walikuwa wanashika nafasi ya pili mpaka ya tatu
na kushindwa kuchukua ubingwa.
Hata Yanga wakishinda mchezo wao wa leo dhidi ya Ruvu
Shooting utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, haitakuwa na
uwezo wa kuifikia Simba, kwani watafikisha pointi 33.
Simba imeshinda michezo 11 iliyompatia pointi 33 na kutoa
sare mechi mbili, zilimfanya kufikisha pointi 35 huku akipoteza mechi mbili.
Post a Comment