TIMU ya Genk ambayo anachezea Mtanzania, Mbwana Samatta leo imejikuta ikilambishwa sakafu yenye pilipili baada ya kukubali kichapo cha mabao 6-0 kutoka kwa Oostende kwenye mchezo wa ligi kuu ya Ubelgiji iliyopigwa jioni ya leo.
Katika mchezo huo ambao Samatta alianza kikosi cha kwanza, ulishuhudiwa wenyeji Oostende wakiandika bao lao la kwanza dakika ya 19 kupitia kwa Franck Berrier, mengine yalifungwa na Antonio Milic (29), Knowledge Musona (56), Nany Dimata alipiga mawili dakika ya 71, 86 mwisho Gohi Cyriac akapigilia dakika ya 83.




Msimamo unaonyesha sasa Genk wapo nafasi ya saba baada ya kushuka uwanjani mara 16 hivyo wamejikusanyia pointi 24.
 

Post a Comment

 
Top