YANGA wana hasira sana. Baada ya kufungwa mabao 2-1 na Mbeya City, Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wamebadili gia lengo likiwa kulipiza kisasi kwa Prisons leo.

Wanajangwani hao leo watakuwa wageni wa Prisons katika mechi ya mzunguko wa 14 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa timu hizo mbili, ambapo kwa vyovyote Yanga watataka kushinda na kufuta machungu waliyoyapata baada ya kufungwa na Mbeya City katika mchezo uliopita.

Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm,  amefanya marekebisho kwenye kikosi chake kutokana na mapungufu aliyoyaona kwenye mchezo uliopita na ana imani ya kuibuka na ushindi katika mechi ya leo.

Pluijm anajua kuwa kikosi chake kikifanya masihara kinaweza kikashindwa kutetea ubingwa wao na sasa hataki tena kupoteza mchezo wa pili mfululizi ndiyo maana anataka ushindi tu hiyo leo.

Yanga ilifanya mazoezi mafupi na ya mwisho jana kwenye Uwanja wa Sokoine, kwa ajili ya mchezo huo, huku Pluijm akitumia muda mwingi kuzungumza na wachezaji wake na kuwaweka sawa kisaikolojia.


Yanga kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 27, nyuma ya wapinzani wao Simba wanaoongoza wakiwa na pointi 35, huku timu hizo zikiwa zimecheza michezo 13 kila moja.
Kikosi kitakachoanza leo ni; 1. Beno Kakolanya
2. Mbuyu Twite
3. Mwinyi Haji
4. Vicent Bossou
5. Kelvin Yondani
6. Thabani Kamusoko
7. Yusufu Mhilu
8. Haruna Niyonzima
9. Donald Ngoma
10. Obrey Chirwa
11. Deusi Kaseke

Akiba
- Ali Mustafa
- Saimon Msuva
- Matheo Antony
- Hassani Kessy
- Vicent Andrew
- Amisi Tambwe
- Nadir Haroub

Post a Comment

 
Top