Zile mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara za
raundi ya Nane Duru la Kwanza, sasa zitafanyika Jumatano.
Michezo hiyo inahusisha timu za Mwadui ya Shinyanga na Azam
FC ambayo ilipewa jina la Mechi Na. 57 itachezwa Uwanja wa CCM Kambarage wakati
Simba itasafiri hadi Mbeya kucheza na Tanzania Prisons katika mchezon Na. 60
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine ilihali Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa
mwenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru jijini katika mchezo Na.59.
Mechi zilipangiwa ratiba, lakini tarehe zake hazikupangwa
(TBA). Tayari Bodi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imewasiliana na wahusika
kuhusu mabadiliko hayo. Sababu ya kuvuta nyuma michezo hiyo ni kutoa nafasi ya
maandalizi ya kambi ya timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri
Ijumaa wiki hii kwenda Harare Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa
unaotarajiwa kufanyika Novemba 13, maka huu.
Post a Comment