LICHA
ya kufanya vuema uwanjani na kufikia hatua ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe
la FA na kufanikiwa kushiriki Kombe la Shirikisho hatua ya makundi, Yanga bado
inaonekana kuifunika timu ambayo ni watani wao, Simba hata nje ya uwanja, hiyo
ni kupitia gharama za usajili kwa mchezaji mmojammoja wa kimataifa.
Nyota
aliyesajiliwa kwa thamani kubwa zaidi ya wote katika kikosi cha Yanga ni Obrey
Chirwa raia wa Zambia ambaye alisajiliwa kwa Sh milioni 240, wakati kwa upande
wa Simba mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi ni Fredric Bragnon raia wa Ivory
Coast aliyesajiliwa kwa Sh milioni 100. Hapo utaona Simba imefunikwa tena kwa
zaidi ya Sh milioni 140.
Post a Comment