UONGOZI wa Yanga umejinasibu kuwa hakuna kanuni
waliyoivunja katika mchakato wa kumsajili beki Hassan Kessy na kudai kuwa unasubiri
hukumu kutoka kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya (TFF) juu ya
mchezaji huyo.
Kauli hiyo imekuja ikiwa ni simu chache baada ya kuwepo
kwa tetesi kuwa Yanga wanaweza kukatwa pointi baada ya viongozi wa timu hiyo
kushindwa kuhudhuria kikao cha Jumatatu kilichoshirikisha kamati hiyo na
viongozi wa klabu hizo.
Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka
Deusdedit alisema: “Sisi hatutakiwi kulizungumzia hilo, tunaiachia kamati, sisi
tulifika katika vikao vitatu lakini Simba wenyewe ambao wenye madai walishindwa
kufika.
“Sisi tunajua
tulichokifanya kwa Kessy, tulimsajili Kessy mkataba wake ukiwa umemalizika,
hivyo hatuna hofu juu ya hilo tusubirie kamati itatoa maamuzi gani baada ya
vielelezo vya timu zote kupitiwa.
“Tulimsajili Kessy rasmi Juni 20, mwaka huu baada ya
kumaliza mkataba wa Simba, Juni 15, mwaka huu, Wanayanga waondoe hofu ya
kupokonywa pointi.”
Post a Comment