WAKALA wa Mario
Baloteli, Mino Raiola amemponda Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp kwa jinsi
alivyokuwa akimtendea straika wake huyo hadi kufikia kuamucha kwenda kujiunga
na Klabu ya Nice ya Ufaransa kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Balotelli,
26, aliachwa na Liverpool katika michezo ya maandalizi ya msimu na kutakiwa
kufanya mazoezi ni wachezaji wa akiba na Klopp akiweka wazi kwamba mchezaji
huyo hakuwa katika mipango yake.
Na Raiola,
ambaye pia anawawakilisha Zlatan Ibrahimovic, Paul Pogba na Romelu Lukaku na baadhi ya mastaa wengine,
hakufuhishwa jinsi mteja wake alivyokuwa akitendewa.
"Mwishoni,
uongozi wa juu wa Liverpool ulikiri kwamba Klopp alikosea," Raiola
aliliambia gazeti la michezo la Italia. Sitaki kumhukumu yeye kama kocha
ingawaje, kwangu, siyo kocha mzuri lakini ameshindwa hata kujua kwamba
Balotelli, pamoja na yote ni binadamu.
"Mario
amekuwa wa kupigiwa mfano. Hajawahi kulalamika alipotakiwa kufanya mazoezi peke
yake. Kusema kwamba ilikuwa ni kosa la Klopp itakuwa ni kejeli."
Raiola
amedai Balotelli alikuwa na uwezo wa kuchagua kubaki sehemu yoyote ya Ulaya
lakini alichagua kwenda Nice akiamini anaweza kurudisha kipaji chake akiwa
Ufaransa baada ya misimu miwili ya kukatishwa tamaa Anfield.
"Kulikuwa
na uwezekano wa kwenda Italia, Ujerumani, au kubaki England, Hispania, lakini
tumechagua Nice," Raiola alisema. Ligi ya Ufaransa ina mvuto na soka lake
la kushambulia.
"Kuhusu
timu ya taifa ni kwamba Mario anaipenda sana lakini sasa mtazamo wake uko Nice.
"Kama
timu ya taifa itamhitaji, ni vizuri, tutafanya mambo mengine, lakini kwa sasa
anafikiria tu kuhusu kurudi uwanjani."
Post a Comment