DIEGO Costa anaamini kwamba anachukuliwa ndivyo sivyo nchini Hispania kuwa yeye ni Mhispania halisi na hachezi katika mojawapo ya klabu kati ya Real Madrid au Barcelona.
Costa ambaye ni straika wa Chelsea, alizaliwa Brazil lakini mwaka 2013 aliamua kuchezea timu ya Taifa ya Hispania.
Muda mfupi baada ya kuichezea Hispania katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ubelgiji na kuiwezesha timu hiyo kushinda mabao 2-0, Costa aliwaambia waandishi wa habari wa Hispania wanamfanyia ndivyo sivyo.

“Ninyi kama waandishi lazima mtambue mchango katika mchezo huu wa kirafiki, nadhani nimefanya vizuri,” alisema Costa na kuongeza:
“Kama ningekuwa nacheza Real Madrid au Barcelona, mngeniambia nimefanya kazi kubwa lakini kwa kuwa mimi si mzaliwa wa Hispania kila muda mmekuwa mkiniponda.
“Sitobadilika na wala sitajali hata kama mkiendelea kuniponda, ni ukweli kuna wakati sifanyi vizuri lakini sihitaji kuandamwa na nawaamini zaidi wenzangu katika timu ambao pia wananiamini.”


Post a Comment

 
Top