Wachezaji
wa Mbeya City ambao walicheza na Toto |
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mwamuzi wa akiba katika mchezo wa Toto African dhidi Mbeya City, Joseph Masija alijikuta ameibiwa simu mbili za mkoni zenye thamani ya Sh 500,000 na fedha Sh 140,000 wakati mchezo ukiendelea.
Mwamuzi huyo aliibiwa vitu hivyo vikiwa katika vyumba vya waamuzi kwenye Uwanjwa wa CCM Kirumba, wakati mchezo huo ukiendelea.
Katika mchezo huo namba 12 mzunguko wa pili katika Ligi Kuu Bara, Masija alikumbana na tukio hilo kwani vyumba hivyo vya waamuzi havina usalama wa kutosha.
Masija alisema ni jambo la kushangaza kuona Bodi ya Ligi inapitisha uwanja huo kutumika katika mechi za ligi hiyo huku ukiwa na upungufu mwingi.
“Nimeibiwa vitu hivyo uwanjani nikiwa nawajibika, hivyo nimewaandikia barua bodi ya ligi wanilipe kwani haiwezekani wapitishe uwanja wenye mapungufu kibao,” alisema Masija.
Naye Kaimu Meneja wa Uwanja wa CCM Kirumba, Mussa Magabe alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema: “Ni kweli awali chumba hicho hakikuwa na kufuli ila sasa tumeweka.”
Post a Comment