Kupitia vyanzo vyetu vya uhakika, imebaini kuwa
thamani ya kikosi kizima cha Yanga ni Sh 1,300,000,000 (Sh bilioni moja na
milioni mia tatu). Hii inamaanisha fedha ambazo zimetumika kuwasajili wachezaji
wote wa kikosi cha kwanza ilionao kwa ajili ya msimu huu wa Ligi Kuu Bara na
michuano mingine.
Wakati
thamani ya kikosi hicho cha Yanga ikiwa hivyo, upande wa pili, thamani ya
kikosi cha Wekundu wa Msimbazi ni Sh 1,003,275,000 (Sh bilioni moja na milioni
tatu laki mbili na sabini na tano).
Hii
ina maana kwamba kama ukilinganisha vikosi hivi viwili, utakutana na ukweli
kwamba Simba inazidiwa kiasi cha Sh 296,725,000.
Post a Comment