BEKI na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amekiri
kuwa sasa ni ngumu kwake kuweza kurejea kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo
kutokana na ushindani uliopo.
Cannavaro ambaye alikuwa kwenye
majeraha ya muda mrefu amekuwa nje katika michezo mbalimbali ya ligi na
kimataifa huko kocha Hans Pluijm akionekana kuwatumia zaidi Yondan na Bossou
katika nafasi ya beki wa kati tofauti na ilivyozoeleka ambapo Yondan na Cannavaro
walikuwa wakicheza eneo hilo.
“Kila kitu kina mwisho wake, huwezi kuwa
kwenye kikosi cha kwanza kwa misimu yote. Kwanza majeraha yamenisumbua sana
halafu kuna watu wapya sasa hivi kwa hiyo sioni tatizo kukaa nje.
Kuna watu wengi wanafanya vyema
kikosini kama dante, Bossou wanafanyakazi nzuri sana.
Wengi walizoea kutuona na
Yondani uwanjani lakini sasa hata tukiwa
hatupo wote kazi inafanyika vyema uwanjani kwa hiyo hakutakuwa na tegemeo
lazima akina fulani wacheze hakuna tena suala la mazoea la wachezaji fulani wacheze,”
alisema Cannavaro.
Post a Comment