TAMASHA la
Kandanda maarufu kama ‘Kandanda Day’, linatarajia kufanyika Oktoba 15, mwaka
huu katika Kiwanja cha Jakaya Kikwete Park (zamani Kidongo Chekundu).
Katika
tamasha la mwaka huu, kauli mbiu itakuwa ni ‘Mpira na Dawati’ kwa maana ya
tamasha hilo kutumika kukusanya fedha
kwa ajili ya kununua madawati yatakayogawiwa kwa shule mbalimbali nchini.
Mratibu wa
tamasha hilo, Mohamed Mkangara, alisema mwaka huu wameamua kuja na kauli mbiu
hiyo, ili kuunga mkono kampeni inayoendelea ya serikali kuhusu uchangiwaji wa madawati
kwa shule za msingi na sekondari.
“Umekuwa ni
utaratibu wetu kila mwaka huu,kuja na kauli mbiu ambayo itahusisha soka na
jambo ambalo moja kwa moja linaihusu jamii, kwahiyo tumeona kwa kutumia soka, tunaweza
kuisaidia jamii yetu kwa urahisi,” alisema Mkangara.
Tamasha hilo
linatarajia kushirikisha timu mbalimbali zilizoalikwa, ukiacha timu wenyeji
Time Dizo Moja na Timu Ismail. Pia siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali na
michezo ya kuvuta kamba kwa washiriki.
Post a Comment