MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Mrisho Ngassa, ana asilimia 90 kurejea Jangwani kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na michuano ya kimataifa mwakani.
Ngassa anatarajiwa Yanga baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa yupo nchini kukamilisha mipango yake, baada ya kuachana na Klabu ya Free State Stars inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini.
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya klabu ya Yanga, zilieleza kwamba Ngassa ana nukia kusaini mkataba kutokana na kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) inaruhusu kwa mchezaji huru licha ya dirisha kubwa la usajili kufungwa Julai 7 mwaka huu.
Chanzo chetu kilisema kuwa tayari kamati ya usajili ya Yanga ipo katika mazungumzo juu ya kumrejesha katika kikosi hicho kinachojipanga kushiriki Ligi ya Mabingwa mwakani.
“Tunamrejesha… amini hilo bado ana nafasi yake katika kikosi chetu,” kilisema chanzo chetu.
Ngassa alishindwa kuweka wazi mipango ya kurejea Yanga zaidi ya kusema anahitaji kuingia dimbani mara kwa mara na kushinda mataji.
“Ninapenda kushinda mataji, nimezoea kushinda mataji tangu nipo mdogo, nina rekodi ya kushinda mataji tangu klabu yangu ya kwanza ya Ligi Kuu Bara (Kagera Sugar).
Ninaondoka Free States kwenda kujiunga na klabu ambayo itanirejesha kwenye enzi za kushinda mataji.”
Post a Comment