KIUNGO Jack
Wilshere akiwa na kikosi chake kipya cha Bournemouth jana alikitumikia kwa mara
ya kwanza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya AC Milan.
Katika
mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa
Vitality ambao ni dimba la nyumbani la Bournemouth, wenyeji hao
walishindwa kutamba kwani walikubali kichapo cha mabao 2-1.
Katika
mchezo huo Wilshere ambaye amejiunga na kikosi hicho kwa mkopo wa msimu mzima
kutoka Arsenal alicheza dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Bao la Bournemouth
lilifungwa na Lys Mousset dakika ya 65, na yale ya AC Milan yakiwekwa kimiani
na Suso (64) na Mbaye Niang (66).
Post a Comment