Mbeya City yatupa kombora Azam
KIKOSI cha Mbeya City kimetamba kuicharaza bila huruma Azam katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, itakayochezwa keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Ofisa Habari wa Mbeya City, Dismas Ten, alisema wataingia uwanjani wakiwa na morali ya hali ya juu baada ya kupata ushindi katika mechi mbili zilizopoita ambazo ni dhidi ya Mbao waliyoshinda 4-1 na Toto African waliyopata ushindi wa bao 1-0.
“Wachezaji wote wapo salama ikiwa na wale ambao hawakusafiri na timu kwenda Mwanza na Shinyanga kwenye mechi zetu tatu za mwanzo tuliikamilisha kwa kushinda miwili na kutoka suluhu mmoja,” alisema Ten.
Ten alisema wanaamini wataifunga Azam, kwani kwa sasa timu hiyo bado haina mwelekeo mzuri, hivyo pointi tatu zote zitabaki kwao na kuendelea kuongoza kwenye ligi.
Alisema wachezaji wanaendelea vizuri isipokuwa mshambuliaji, Geofrey Mlawa, ataikosa mechi hiyo kutokana na kuwa majeruhi aliyoyapata dhidi ya Toto Africans.


Post a Comment