Wachezaji wa Lyon
|
Huu utakuwa mchezo wa pili kwa JKT baada ya awali kuwabana Simba na kutoka nayo suluhu wiki iliyopita wakati Lyon wenyewe watakuwa wakicheza mchezo wa tatu, wa kwanza walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam kasha wakapigwa 3-0 na Yanga.
Ofisa Habari wa JKT Ruvu, Constantine Masanja, amesema wamejiandaa vizuri dhidi ya mchezo huo na kudai kuwa wanauhakika wa kushinda na kuzoa pointi zote tatu zitakazowaweka pazuri kwenye msimamo wa ligi.
Masanja amesema kuwa, awali walijiandaa na mchezo dhidi ya Yanga ambao ulikuwa uchezwe Jumanne ya wiki hii kabla ya kuahirishwa kutokana na Taifa Stars kuwa na ratiba ya kucheza dhidi ya Nigeria, hivyo hasira zote watazimaliza kwa Lyon hii leo.
Post a Comment