KAMA umewahi kushuhudia mechi yoyote ya Yanga ikimalizika wachezaji wake hufanya nini, basi taarifa ikufikie wewe kwamba Simba nayo imekuja na mtindo huo lengo likiwa ni kujiweka fiti zaidi.
Nadhani unajua, lakini kama hujui ipo hivi, tangu Yanga iwe na kocha msaidizi, Juma Mwambusi aliyetokea Mbeya City, imekuwa na kawaida ya kufanya mazoezi mepesi baada ya kumaliza mechi, hali hiyo pia Simba wanayo kwa sasa.
Simba ambayo kwa sasa inajifua vikali kwenye kambi yao iliyopo mkoani hapa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, tayari imeshacheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya Polisi Moro, Moro Kids na Burkinafaso ambapo mechi hizo zote imeibuka na ushindi.
Kila baada ya kumaliza mechi, imekuwa na kawaida ya wale wachezaji waliomaliza mchezo kunyoosha viungo kabla ya kwenda kupumzika.
Championi limekuwa likishuhudia hali hiyo kila kwenye mchezo na anayeongoza mazoezi hayo ni kocha msaidizi, Mganda, Jackson Mayanja hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa kocha huyo kuitumia staili hiyo.

Post a Comment

 
Top