KAMPUNI ya
Wachina ya Beijing Construction and Engeenering Group leo imeukabidhi rasmi Uwanja
wa Uhuru kwa Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye kwa niaba
ya Serikali baada ya kukamilika kwa marekebisho yake yaliyoanza miaka mitatu
iliyopita.
Marekebisho
hayo yaliyoanza mwaka 2013 yameigharimu Serikali shilingi 12 Bilioni na sasa
uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 23,000 walioketi.
"Niwaombe
wadau waendelee kuiunga mkono Serikali kwa kuwekeza kwenye michezo ili kuifanya
nchi yetu kufanya vizuri zaidi kimataifa," alisema Nape.
Kwa upande
wake Katibu mkuu wa Wizara ya Habari Elisante Ole Gabriel alimuhakikishia
Waziri Nape kuwa miundo mbinu ya uwanja huyo italindwa ili iendelee kudumu
zaidi kama matakwa ya Serikali.
Katika hatua
nyingine Katibu mkuu huyo amepiga marufuku uwanja huo kuitwa 'Shamba la Bibi' kutokana
na historia kubwa ulionao kwa Taifa hili tangu nchi ilipopata Uhuru.
Post a Comment