KOCHA
Joseph Omog amechukua uamuzi wa kuzungumza na Laudit Mavugo muda mfupi baada ya
mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC, Jumamosi iliyopita ambapo Simba
ilishinda kwa mabao 3-1 lakini Omog hakufurahishwa na aina ya uchezaji wa
kucheza kama yuko peke yake uwanjani.
Kocha
huyo amemuonya Mavugo kuwa anatakiwa kuhakikisha anawapa pasi wenzake na
kucheza kitimu badala ya kuwa mbinafsi.
“Sitaki
kuwa na mchezaji mbinafsi, ninataka kuona wachezaji wote wakicheza kitimu kwa
washambuliaji kutengenezeana nafasi ya kufunga, mabeki kulinda goli na viungo
kuchezesha timu.
“Baada
ya mchezo wa Ndanda niliwaita wachezaji wote nikazungumza nao na kuwaambia
ninataka umoja na ushirikiano kama timu, sitaki mchezaji akiendelea kucheza na
jukwaa kwa lengo la kuwafurahisha mashabiki huku mipango ikiharibika.
“Mfano
Mavugo kuna nafasi mbili alipata angeweza kumpa Ajib akafunga na nyingine
alipata akashindwa kumpa (Fredric) Blagnon akafunga.
“Jambo
zuri ni kuwa Mavugo alinielewa na kukiri kosa ambapo pia aliwaomba msamaha
wenzake na kuahidi kubadilika kwenye mechi zijazo,” alisema Omog.
Post a Comment