WAKATI Yanga kesho Jumapili ikitarajiwa kushuka
uwanjani
kupambana na African Lyon katika mchezo wake wa kwanza
wa Ligi Kuu
Bara msimu huu, jana mwenyekiti wa klabu hiyo,
Yusuf Manji alifanya kikao
kizito cha dakika 270 na wachezaji
wa kikosi hicho.
Kikao hicho maalum kilifanyika kwenye ofisi za tajiri huyo
zilizopo jengo
Quality Plaza jijini Dar. Kikao hicho kilianza
saa 2:00 asubuhi hadi saa 6:30
Mchana.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zimedai kuwa,
kikao hicho
kilikuwa maalumu kwa wachezaji pamoja na
viongozi wa benchi lao la ufundi ambapo walipata kujadili
mambo mbalimbali
yanayowahusu, likiwemo suala la ushiriki wao kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu
ambao wanakabiliwa na
changamoto kubwa ya kutetea ubingwa wao.
“Ni kweli kabisa wachezaji wetu walikuwa na kikao na
mwenyekiti kwa ajili
ya kuzungumza mambo mbalimbali
yanayowahusu lakini pia ushiriki wao katika
michuano ya ligi kuu.
“Kama unavyojua siku chache zilizopita walipatwa na
hofu kubwa baada ya
taarifa kuwa mwenyekiti anataka
kuachana na timu kutokana na kuchoshwa na
matusi ambayo
amekuwa akikumbana nayo tangu siku aliyotangaza kutaka
kuikodi
timu yetu.
“Kutokana na hali hiyo, pia ametumia mkutano huo kuwaondoa
hofu hiyo
waliyokuwa nayo wachezaji wetu na amewataka
wapige kazi kwani ushindani msimu
huu ni mkubwa na yeye
yupo nao bega kwa bega kuhakikisha wanawatimizia mahitaji
yao yote, ikiwa ni pamoja na stahiki zao wanazostahili kupewa
kulingana na
makubaliano yao,” kilisema chanzo hicho cha
habari na kuongeza:
“Mambo sasa yamekaa sawa, hivyo ile hofu ya kufanya vibaya
msimu huu
ikiwa ni pamoja na mchezo wetu wa kwanza dhidi
ya African Lyon imeondoka, hivyo
Wanayanga tushikamane
pamoja ili kuhakikisha hatuvurugani tena.”
Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit ili aweze kuzungumzia
suala hilo, hakuweza kupatikana kufuatia simu yake ya mkononi kuita tu bila ya
kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe
wa maandishi hakuweza kujibu.
Hata hivyo, walipoulizwa kuhusiana na suala hilo, baadhi ya
wachezaji wa
timu hiyo ambao waliomba kutotajwa majina yao
gazetini walisema: “Taarifa hizo
ni za kweli kabisa kwani ilikuwa tukutana naye jana (juzi) lakini baadaye
tulipewa taarifa kuwa
amechoka na leo (jana) ndiyo tumekutana naye.”
Post a Comment