KIKOSI cha
timu ya taifa ya Serengeti Boys kimefanikiwa kutinga hatua inayofuata kwenye
michuano ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Afrika kwa Vijana baada yta
kuifunga Afrika Kusini mabao 2-0.
Katika mchezo
wa awali uliopigwa huko Afrika Kusini, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 kabla
ya leo kurudiana kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar hivyo matokeo ya jumla kuwa 3-1.
Serengeti
ambayo ilionyesha soka zuri ilifanikiwa kuandika bao la kwanza dakika ya 33
kupitia kwa Mohamed Rashid Abdallah kisha Muhsin Makame katika dakika ya 85 bao
ambalo lilionekana kuwamaliza nguvu wageni hao.
Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo , Nape Nnauye alikuwepo uwanjani hapo
kuwapa sapoti vijana hao ambao pia hawakumuangusha.
Katika
mchezo huo, mchezaji wa Serengeti Boys, Ally Ng’anzi alipata kadi nyekundu
katika hatua za mwisho kuelekea kukamilika kwa kipindi cha kwanza lakini hiyo
haikupunguza nguvu ya Watanzania hao.
Serengeti
sasa itakutana na kati ya Namibia au Congo Brazzavile na ikishinda itatinga
fainali ya michuano hiyo itakayofanyika mwakani nchini Madagascar.
Post a Comment