Muimbaji wa
‘Na Yule’ Ruby amesema hakwenda Mwanza kutumbuiza kwenye Fiesta licha ya
‘kusajiliwa’ kwenye msimu mpya wa tamasha hilo maarufu, kwasababu waandaji
hulipa fedha ‘kiduchu.’
Kauli yake
inakuwa mkuki kwenye moyo kwa Clouds FM ambao ndio waliomfikisha hapo alipo kwa
kukivumbua kipaji chake.
Akiongea na
tovuti ya Tizneez, Ruby alidai kuwa kutolewa kimuziki na Clouds Media,
hakumaanishi kuwa ataendelea kuwatumikia kama wanavyotaka kwakuwa naye ana
maisha yake kwa sasa.
“Kisa ni
Clouds ndio nisiwe free na kuongea?” alihoji muimbaji huyo ambaye kwa miaka
mingi sauti yake imekuwa ikisikika kwenye matangazo kibao ya kituo hicho
maarufu cha redio nchini. Amedai kuwa show ya Fiesta ni kubwa kuliko maslahi
wanayolipa na kwamba yangemwacha katika wakati mgumu kuandaa show yake.
Anadai kuwa
hahofii vita yoyote na kituo hicho chenye nguvu kilichowahi kuingia kwenye
mgogoro na wasanii kibao ambapo wapo walio kubali yaishe kwa kupiga magoti na
kuomba msamaha, isipokuwa Lady Jaydee ambaye bado ana vita nao iliyodumu kwa
miaka mingi.
Ruby anasema
mwisho wa siku ni maisha yake ndiyo ya muhimu zaidi. Ruby alipatikana kupitia
shindano la Supa Diva liliondaliwa na Clouds kupitia tamasha la Fiesta na
kusainishwa chini ya kampuni ya THT iliyoanzishwa na Ruge Mutahaba.
“To be
honest naumia sana sababu they don’t care,” anasema. “So if someone hakujali,
what can you do? Tatizo ndio kama hilo unakuwa na management ambayo haijali
maslahi yako kwenye maisha yako. Tunajikuta tunakuwa na management ambazo
zinajali umabavu, zinaendesha wasanii kimabavu kuliko kiakili ya kutimiza
malengo ya wasanii wao ambapo sisi wasanii wa kike tunaonewa sana. Unadhani
kwanini Lady Jaydee wanamuita komando?” amehoji Ruby.
“Because ni
mtoto wa kike, ni mwanamke ambaye amesimama kweli kweli na kujitetea, lakini
wachache sana wanafanya hivyo.”
Kukiwekea
kidonda chumvi, Ruby ambaye kwenye Instagram amepost video akiimba wimbo wa
Lady Jaydee, amedai kuwa ana mpango wa kufanya naye kazi. “Nitafanya naye
sababu ni muimbaji mzuri, ana sauti nzuri.”
CHANZO:
Bongo 5
Post a Comment