SIMBA ilikuwa ikimsubiri kwa
hamu kipa wa Azam FC, Mwadini Ali ambaye ilielezwa angekwenda kwa mkopo,
sambamba na fowadi, Ame Ally ‘Zungu’, hata hivyo dili la Mwadini liliyeyuka
ghafla na sasa kipa huyo anadunda ndani ya Azam.
Hata hivyo, imebainika kuwa
chanzo kikuu cha kugeuzia gia angani ni kipa Muivory Coast, Daniel Yeboah
ambaye walikatisha mpango wa kumsajili mwishoni kabisa mwa usajili na kuamua
kuimarisha zaidi safu za ndani hivyo kubatilisha mpango wa kumtoa Mwadini.
Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad
Kawemba amekiri kuwa mpango wa kumtoa kipa huyo kwa mkopo ulikuwepo wakati Ame
anatua Msimbazi lakini wakabadili maamuzi ghafla, hivyo Muivory Coast kuachwa
yeye pamoja na Mhispania, Gonzalez Jesus waliyokuja majaribioni.
“Kweli Mwadini alikuwa aende
Simba lakini baadaye tuliamua kumbakisha na akachukua nafasi ya Daniel ambaye
tuliachana naye ili tuimarishe zaidi nafasi za ndani katika usajili wa
wachezaji wa kigeni,” alisema Kawemba.
Nyota wapya wa kikosi hicho
ni Frasicsco Zekumbariwa (Ivory Coast), Daniel Amoah (Ghana), Golanzo Ronardo
(Ivory Coast), Bruce Kangwa (Zimbabwe) na Enock Agyei (Ghana-aliyeachwa kwa
mkopo Medeama). Wanaungana na Kipre Bolou (Ivory Coast), Jean Mugiraneza
(Rwanda) na Pascal Wawa (Ivory Coast).
Post a Comment