HUENDA washambuliaji wa zamani wa Simba Mganda, Emmanuel Okwi na Mbwana Samatta, wakakutana kwenye michuano ya Europa League, ila mara hii kila mmoja akiwa na timu yake.

Wawili hao wanaweza kukutana kama timu zao zitafanikiwa kumaliza vizuri mechi zao za mwisho zilizobaki na kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Samatta anaichezea Genk ya Ubelgiji na Okwi anaichezea  SonderjyskE ya nchini Denmark, ambapo timu hizo zipo kwenye nafasi nzuri za kutinga hatua ya makundi ambayo huenda zikajikuta zikipangwa kundi moja.


 Katika mchezo wao uliopita Genk walilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na Lokomotiva Zagreb ya Croatia huku Samatta akifunga bao moja na sasa wanasubiri mchezo wa marudiano nyumbani Alhamis ijayo ambapo kikosi hicho kinatakiwa kushinda au sare ya bao 1-1 au suluhu ya 0-0.

Kwa upande wa kikosi cha akina Okwi, walilazimishwa suluhu ya 0-0 dhidi ya Sparta Praha ya Jamhuri ya Czech, nyumbani na sasa wanatakiwa kupata ushindi wowote au sare yoyote ya mabao ili kutinga hatua ya makundi.

Post a Comment

 
Top