BEKI wa
pembeni wa Yanga, Hassan Kessy, amesema miongoni mwa mechi alizokuwa anatamani
kucheza basi ni hii dhidi ya TP Mazembe itakayochezwa kesho Jumanne na ameahidi
kupiga soka la nguvu.
Yanga ambao
wameondoka jana asubuhi kuelekea DR Congo, kesho Jumanne wanatarajiwa kuvaana
na Mazembe kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Beki huyo
alizikosa mechi za awali za Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na utata kwenye
usajili wake kutoka Simba kwenda Yanga lakini baada ya kuruhusiwa kuichezea
Yanga wikiendi iliyopita, ameonekana kuwa mwenye furaha.
Akizungumza na
Championi Jumatatu, Kessy alisema alikuwa ana shauku kubwa ya kuichezea Yanga
katika michuano ya kimataifa, hivyo baada ya TFF kumruhusu, basi mechi hiyo
ataitumia kujitangaza kimataifa ili afungue milango ya kucheza soka nje ya
nchi.
Aliongeza
kuwa, licha ya mwaka huu kuzikosa baadhi za mechi za kimataifa, amepania
kuonyesha kiwango kikubwa wakati timu yao itakapovaana na Mazembe.
“Mimi kitu cha
kwanza kabisa kilichonileta Yanga ni michuano ya kimataifa, baada ya timu yangu
hii mpya kushiriki, nikiamini hapa ndiyo sehemu sahihi kwangu kutimiza malengo
yangu ya kucheza soka nje ya nchi. Hivyo basi nimepanga kuonyesha kiwango
kikubwa kwenye mechi hii yangu ya kwanza kimataifa na Mazembe.
"Ninajua
mechi hii haina umuhimu kwetu kwani tayari baada ya kupoteza michezo ya
mwanzoni tumetolewa, lakini kikubwa heshima, hivyo ni lazima tupambane ili
tupate ushindi wa ugenini," alisema Kessy.
Post a Comment