mavugo |
KOCHA wa Simba, Joseph Omog, amewaweka kitimoto mastraika
wake Mrundi, Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib na kuwataka kuacha ubinafsi
wanapokuwa uwanjani na badala yake wacheze kwa kushirikiana na mwenye kuzingua
benchi litamhusu.
Kuelekea kwenye pambano la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
dhidi ya JKT Ruvu litakalochezwa kesho kwenye Uwanja Taifa, Dar es Salaam, Omog
ameona awaweke chini mastraika wake hao tegemeo na kuwataka kuacha uchoyo
uwanjani na kucheza kwa ajili ya timu na si mafanikio binafsi.
Omog aliwapa onyo hilo mastaa hao wawili wa Simba baada ya
kuwatazama kwenye mechi ya kwanza ya Ligi Kuu na zile mbili za kirafiki dhidi
ya AFC Leopards na URA na kugundua kuwa kila mmoja amekuwa akicheza kichoyo
anapokuwa uwanjani.
Kocha huyo wa zamani wa Azam, alionekana kuchukizwa na tabia
ya Mavugo na Ajib kucheza kichoyo wakati timu yake ikiwa inahitaji ushindi kitu
ambacho kinaweza kuwaumiza siku za usoni.
Ajib katikati
|
Akizungumza na BINGWA, Omog alisema amewaweka chini
mastraika hao wawili na kuwapa onyo kali huku akisisitiza kuwa mchezaji ambaye
ataendelea na tabia hiyo ya uchoyo kumsugulisha benchi au kumtoa uwanjani kama
akiwa anacheza.
“Timu kwanza mtu baadaye, hakuna ubinafsi kama mtu anajiona
yeye ni mbinafsi aachie ngazi wengine wafanye kazi, hatupo hapa kujionyesha
kila mtu anaweza,” alisema Omog.
Alisema kitendo cha mastraika hao wawili kucheza na kunyimana
pasi katika mchezo uliopita dhidi ya Ndanda FC kulilipa wakati mgumu benchi la
ufundi la timu hiyo katika kipindi chote cha dakika 90 za mchezo huo.
“Tulikuwa tuna uwezo wa kufunga mabao zaidi ya matano siku
ile, lakini kwa tabia zao za kunyimana pasi na kucheza kibinafsi kulitupa
wakati mgumu sana pamoja na kuwa tulishinda mchezo ule,” alisema Omog.
Aliongeza kusema kuwa Simba msimu huu imedhamiria kufanya
kweli ndio maana benchi la ufundi la timu hiyo limeweza kusajili kikosi kipana
kilichosheheni lundo la wachezaji wenye vipaji vya hali juu.
“Hakuna Mungu mtu, nina washambuliaji wengi kama Fredrick
Blagnon, Danny Lyanga na Ame Ali kwa hiyo atakayeshindwa kwenda na sera zetu
aachie ngazi mapema,” alisisitiza Omog.
Simba kesho itashuka katika dimba la Taifa jijini Dar es
Salaam kuwavaa maafande wa JKT Ruvu ikiwa ni mchezo wao wa raundi ya pili ya
Ligi Kuu Tanzania Bara.
Post a Comment