LICHA ya
ubora wa picha angavu, bado Kampuni ya Azam TV imeona haitoshi na kuamua
kuongeza vifaa vya kisasa zaidi pamoja na kufanyia marekebisho changamoto zote
walizokumbana nazo msimu uliopita katika kurusha matangazo ya Ligi Kuu Bara.
Ikumbukwe
kuwa Azam TV, wiki kadhaa iliingia mkataba wa miaka mitano na Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) wenye thamani ya Sh bilioni 23 kwa ajili ya matangazo ya
Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza leo Jumamosi katika viwanja tofauti.
Kaimu
Mkurugenzi wa Azam Media, Tido Mhando, amesema kuelekea msimu mpya, wameboresha
huduma zao ikiwemo gari la kisasa la matangazo (Ob Van), kila mechi kuwa na
kamera si chini ya sita na kujenga majukwaa ya muda katika baadhi ya viwanja
vyenye miundombinu mibovu ili kupata picha nzuri.
“Awali kuna
baadhi ya viwanja tulipata shida sana ya kupata picha bora kutokana na
miundombinu ya viwanja lakini hilo tumelikabili. Tumeongeza gari la Ob Van la
kisasa na bora zaidi Afrika nzima, hivyo tunatarajia kuwa na picha zenye ubora
wa hali ya juu,” alisema Mhando.
Post a Comment