KOCHA wa Klabu
ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza, Mauricio Pochettino amemsifia kiungo wake
mkabaji, Mkenya Victor Wanyama na
kumfananisha kama "mnyama".
Kocha huyo
amesema mchazji huyo ana uwezo mkubwa uwanja pamoja na nguvu vitu ambavyo
anaamini vitaisadia timu hiyo msimu huu kwenye ligi na michuano mingine
mbalimbali.
"Ni
mnyama, ninamfahamu vyema kwa sababu nilimnunua nikiwa Southampton kutoka
Celtic. Ni rahisi sana kutambua sifa hizi," alisema kocha huyo wakayi
akijibu maswali kuhusiana na umuhimu wa mchezaji huyo kwenye kikao na waandishi
wa habari huko Londo.
Pochettino,
raia wa Argentina, alianza kuifundisha Spurs Mei 2014 ambapo alipewa mkataba wa miaka mitano kabla
ya Mei mwaka huu tena kuongeza kandarasi ya miaka mitano ambayo itamalizika 2021.
Wanyama ametua
Spurs msimu huu akitokea Southampton kwa dau la pauni milioni 11 ambapo
alijiunga kwa mara nyingine na kocha wake huyo kwani awali Pochettino wakati
akikinoa kikosi cha Soton alimsajili Wanyama kutoka Celtic kwa dau la pauni
milioni 12.5.
Post a Comment