IKICHEZA
mchezo wa pili kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu huu, Mbeya City jana
imefanikiwa kuvuna pointi zote tatu muhimu baada ya kuifunga Toto Afican ya
Mwanza bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.
Haruna
Shamte lifunga bao hilo mapema dakika ya saba kwa mpira wa adhabu iliyotolewa
baada ya Joseph Mahundi kuangushwa alipokuwa akijaribu kuwatoka walinzi wa Toto
African, hii ilikuwa ni baada ya mashambulizi mfululizo ambayo City iliyafanya
kwenye lango la timu hiyo ya Mwanza tangu kipenga cha kuanza mpira kilipopulizwa.
Raphael
Daud, Kenny Ally na Joseph Mahundi walicheza vizuri kwenye eneo la kiungo na
kuifanya City kung’ara vizuri uwanjani kipindi chote cha kwanza licha ya
jitihada za mara kadhaa kutoka kwa wachezaji wa Toto.
Baada ya
mchezo huo kumalizika Kocha wa Mbeya, Kinnah Phiri alisema: “Vijana wangu
wameonyesha mchezo mzuri, kama ilivyokuwa kwenye mchezo uliopita, kitu izuri
zaidi ni kuwa leo tumepata pointi tatu, hili ni jambo jema, kwa sababu tunapata
nguvu ya kupambana kwenye mchezo ujao.”
Mbeya City
sasa jumla wamekusanya alama nne kutoka kanda ya ziwa katika michezo miwili
waliyoshuka dimbani, awali walitoka sare na Kagera Sugar ambayo inatumia uwanja
wa Kambarage, Shinyanga.
Post a Comment