KOCHA Msaidizi wa Simba,
Jackson Mayanja, amekiri kuwa aliweka asilimia zote kuwa Yanga ingeifunga Azam
katika mechi yao ya juzi ya Ngao ya Jamii lakini ameshangazwa na kilichotokea,
Azam kuifunga Yanga.
Azam iliifunga Yanga kwa
mikwaju ya penalti 4-1 baada ya matokeo ya sare ya 2-2 katika dakika 90 za
mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
“Sikutegemea kama Yanga
ingefungwa na Azam, niliweka asilimia kubwa za Yanga kuibuka na ushindi maana
imekaa kwa pamoja muda mrefu tangu ligi imeisha, hakuna mabadiliko makubwa na
wachezaji wamekuwa na uzoefu mkubwa sasa zaidi ya wachezaji wa Azam kutokana na
mechi zao za kimataifa.
“Hata mpira wa uwanjani Yanga
ilionekana kuwazidi Azam kwa kiwango kikubwa lakini mwisho matokeo yamekuwa
kama yalivyoonekana, lakini hiyo ndiyo hali halisi ya mpira, nafikiri kuna cha
kujifunza hapo,” alisema Mayanja.
Post a Comment