IKIWA inaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa ligi
kuu dhidi ya Mbao Fc uliopangwa kuchezwa
mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mbeya City fc inataraji kuondoka mjini Shinyanga ijumaa hii kuelekea jijini Mwanza tayari kwa
kuikabili timu hiyo iliyopanda
daraja kwa ‘mtereko’ tiketi ya mezani.
Mapema leo kwenye
uwanja wa Kambarage wakati wa mazoezi ya
asubuhi afisa habari wa kikosi hiki,
Dismas Ten, amesema kuwa City
itaondoka mjini Shinyanga ijumaa
jioni kuelekea jijini Mwanza ikiwa na lengo moja tu la kuvuna pointi tatu zingine kwenye uwanja wa CCM Kirumba kama
ilivyokuwa kwenye mchezo wa juma lililopita dhidi ya wenyeji Toto
Africans.
“Tumekuwa hapa Shinyanga
toka siku ya jumatatu, kwa ajili
ya mazoezi na matayarisho ya mchezo wa jumamosi,Mwalimu alichagua kufanya mazoezi Kambarage kwa lengo moja tu la kupata utulivu na
kuandaa kikosi vizuri ili kuhakikisha tuanshinda na kupata pointi tatu kwenye siku nzuri ya
Septemba 3 , kikosi chetu kiko sawa, pasipo majeruhi yeyote na tunakwenda
Mwanza kucheza kwenye uwanja ambao siku
zote tumekuwa na bahati nao”. alisema
Akiendelea zaidi Ten
aliweka wazi kuwa kiungo Geoffrey Mlawa
na mshambuliaji Omary Ramadhani waliyopata majeraha kwenye mchezo uliopita dhidi ya Toto Africans wamerejea kwenye
hali nzuri na anaweza kuwa sehemu ya mchezo huo wa jumamosi endapo
Mwalimu Kinnah Phiri atapenda kuwatumia.
“Dakika 90 zilizopita tulizihitimisha kwa kupata majeruhi
wawili kwa Omary Ramadhani na Geoffrey Mlawa, jopo la madaktari wamethibitisha kuwa wachezaji hao wako sawa na wanaweza kucheza
kwenye mchezo wa jumamosi ingawa jambo hilo
litategemea na maamuzi ya mwalimu, kuwepo kwao kikosini kutaongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji
ambalo ni muhimu kwenye kusaka pointi tatu,hasa ukizingatia kiwango kizuri
walichokionyesha kwenye mechi dhidi ya Toto Africans” alimaliza
Post a Comment