STRAIKA mpya wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo,
amewaomba mashabiki wa timu hiyo wasimhukumu kwa lolote lililotokea Uwanja wa
Taifa juzi walipoifunga Ndanda 3-1 huku akisisitiza kuwa ndiyo kwanza ameanza
kazi.
Hata hivyo, straika huyo amewaomba radhi
mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kuonekana kuwa mchoyo uwanjani katika
nafasi ambazo wenzake wangeweza kufunga.
Mavugo ambaye alifunga bao la kwanza katika
ushindi huo katika mchezo huo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam, amesema: “Nawaomba wapenzi na mashabiki wasiwe na hofu
yoyote dhidi yangu kutokana na kutoonyesha kiwango kizuri katika mchezo huo kwa
sababu kulikuwa na mambo najifunza lakini ni matumaini yangu kuwa mechi zijazo
nitakuwa bora zaidi ya nilivyocheza.
“Nawaomba watulie na wasiwe na wasiwasi na mimi
nitawafanyia kazi na nitahakikisha ninafunga kila mechi endapo Mungu atapenda
kwa sababu tayari nimeshaiona ligi ya Tanzania ikoje na ninatakiwa nichezeje.”
Mavugo amejiunga na Simba hivi karibuni akitokea
Vital’O ya Burundi na hadi sasa ameshaifungia mabao mawili katika mechi tatu
moja ya ligi na mbili za kirafiki.
Post a Comment