MSHAMBULIAJI wa Simba,
Mrundi, Laudit Mavugo, amefunguka kwamba anachokiwaza kuwafanyia mashabiki na
viongozi wa timu hiyo ni kuipa ubingwa klabu hiyo.
Mavugo ambaye ametua klabuni
hapo hivi karibuni akitokea Burundi baada ya kufeli majaribio ya kucheza soka
la kulipwa katika timu ya Tours inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Ufaransa, amesaini
mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba na tayari ameonyesha kiwango
kilichowafurahisha Simba.
Mavugo anayevaa jezi namba
tisa, alisema ubingwa ndilo jambo pekee analoliwaza kwa sasa, kwamba ni jinsi
gani ataiwezesha timu hiyo kufanikisha mpango huo.
“Ni lazima nijitume na
kuonyesha kiwango kikubwa na kufunga mabao ambayo yataipa mataji timu yangu,
kwa sababu kwanza hilo ni jukumu ambalo natakiwa kulifanya lakini kingine ni
kuwapoza mashabiki ambao walikuwa na hamu na mimi.
“Kama sitaisaidia Simba
kutwaa ubingwa wa ligi au kombe lolote lile, nitakuwa sijatekeleza kile ambacho
nimedhamiria kukifanya hapa na naamini mambo yote yatawezekana kwa sababu
naungwa mkono kwenye kila kitu ambacho nakifanya,” alisema Mavugo ambaye alikuwa
akiichezea Vital’O ya Burundi.
Post a Comment