KUNGO wa Manchester United, Ander Herrera
amesema kuwa safari hii hawatafanya utani na badala yake wataichukulia michuano
ya Europa League kwa umakini mkubwa tofauti na ilivyokuwa awali.
Man United ipo katika michuano hiyo kutokana
na kumaliza msimu katika Premier League ikiwa katika nafasi ya tano huku ikiwa
na kumbukumbu mbaya ya michuano hiyo.
Man United ilitolewa na Athletic Bilbao katika
hatua ya 16 Bora mwaka 2012 pia msimu uliopita ilitolewa na Liverpool katika
hatua hiyohiyo.
"Nafikiri ni michuano mizuri na tunataka
kushinda, Europa League imekuwa michuano muhimu kila msimu na imepata umaarufu.
“Sisi ni klabu kubwa na tunaheshimu wapinzani
wetu lakini tutapambana ili tuwe mabingwa, tuna kikosi kizuri, tunao wachezaji
wanaoweza kucheza Alhamisi, Jumapili, Alhamisi na Jumapili tena,” alisema
Herrera.
Post a Comment