KOCHA Mkuu
wa Yanga, Mholanzi Hans Pluijm, amefichua uozo uliofanywa na wachezaji wake
mpaka ikafanya vibaya kwenye michuano ya kimataifa, huku akisema kadi
walizopewa Donald Ngoma na Thabani Kamusoko zilichangia.
Yanga ambayo
jana Jumanne ilikamilisha ratiba yake ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kucheza
dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo, haikuwa na msimu mzuri kwenye michuano hiyo
hali iliyowashusha morali ya mashabiki wake.
Kabla ya
mchezo wao wa jana, Yanga ilikuwa tayari imeshacheza mechi tano dhidi ya MO
Bejaia, Medeama na TP Mazembe na kufungwa tatu, sare moja na kushinda moja,
ikikusanya pointi nne.
“Ni lazima
tulipaswa kupata ushindi kwenye mechi za nyumbani, pia tulifanya makosa mengi
kwenye safu yetu ya ulinzi na hiyo ndiyo ilitufanya tufungwe mabao ambayo
mengine ni ya kizembe.
“Kiukweli
mechi za nyumbani ni lazima ushinde, usipofanya hivyo kwako unadhani utawezaje
ugenini, yote kwa yote huu ni mpira, tunakubali matokeo ya aina yoyote yale.
Katika hatua
nyingine, Pluijm alisema kitendo cha kuwakosa mara kwa mara wachezaji wake
ambao wengi walikuwa ni watovu wa nidhamu na kulazimika kukosa mechi kutokana
na kutumikia kadi za njano na nyekundu kilichangia hali hiyo.
Ikumbukwe
kuwa, katika mechi hizo zote mpaka Yanga inamaliza mchezo wake wa jana,
iliwakosa Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima,
Vincent Bossou na Kelvin Yondani, ambao walikuwa na kadi mbili za njano huku
Haji Mwinyi, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wakikosa baadhi ya mechi kwa kuwa na kadi
nyekundu.
Post a Comment