Kocha mkuu
wa timu ya Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametaja kikosi cha wachezaji 20
kwa ajili ya pambano la kukamilisha ratiba ya mechi za kuwania kufuzu Kombe la
Mataifa ya Afrika.
Kuna
mabadiliko machache katika kikosi hicho ukilinganisha na uteuzi uliopita
kutokana na majeruhi na kushuka kwa viwango.
Mshambuliaji
Thomas Ulimwengu pamoja na beki wa kulia, Juma Abdul wameachwa kutokana na
majeruhi.
Kiungo
Mwinyi Kazimoto ametemwa na nafasi yake kuchukuliwa na chipukizi Muzamiru
Yassin wa Simba.
Simon Msuva
pia amerudishwa katika kikosi huku David Kaseke akitemwa.
Kikosi
Kamili:
Makipa:
Deogratius Munishi, Aishi Manula.
Walinzi:
Kelvin Yondani, David Mwantika, Vincent Andrew,
Shomari Kapombe, Mwinyi Haji, Mohamed Hussein.
Viungo:
Jonas Mkude, Himid Mao, Muzamiru Yassin, Shiza Ramadhan, Farid Mussa, Simon
Msuva.
Washambuliaji:
John Bocco, Mbwana Samatta, Ibrahim Ajib.
Post a Comment