KIKOSI
CHA SIMBA KINACHOANZA LEO V JKT RUVU
DAK 2: simba wanaonekana kumiliki mpira hususan eneo la kiungo na JKT wanaonekana kuzuia muda mwingi
Dk 7: JKT Ruvu wanaonekana kuamka sasa na wanafika langoni
mwa wapinzani wao. Simba inaonekaana
kutokuwa makini zaidi hasa wanapolifikia lango la wapinzani wao huku wkaipoteza
mipira mingi nje ya 18.
DK 13 Mavugo anafanyiwa faulo nje kidogo ya 18, na anapiga
mwenyewe faulo hiyo lakini shuti lake linapaa kidogo nje ya lango la JKT Ruvu
Mchezaji wa JKT Ruvu anashindwa kufunga bao la wazi kabisa kufuatia kumpiga chenga kipa na kisha lango kubaki na
mabeki wa Simba ambao wameokoa. Mechi bao 0-0
Dk 22. Kichuya almanusura awape Simba bao la kuongoza
kutokana na shuti lake kali alilopiga nje ya 18 kupanguliwa kiufundi na kipa wa
JKT na kuwa kona ambayo haijazaa matunda
Dk 35:
Kichuya anawapiga chenga mabeki watatu wa JKT ndani ya 18 akitaka kwenda
kufunga lakini hata hivyo chelewachelewa yake inawafanya mabeki wa maafande hao
wamuwahi na kuutoia mpira kwenye hatari.
Kipindi cha pili kimeanza
DK 45; za kipindi cha kwanza
zimemalizika Simba 0-0 JKT Ruvu
punde tutawaletea uchambuzi wetu Kipindi cha pili kimeanza
Dk 51: Jamal
Mnyate anatoka anaingia Miwnyi Kazimoto
DK 65: Anatoka Blagnon anaingia Ajib
Simba wanaonekana kusaka bao kwa
nguvu lakini kila wanapolikaribia lango la wapinzani wamekuwa wakishindwa
kujipanga vyema
JKT sasa wanaonekana kucheza pasi za
kugongeana
DK 70 Offside MAvugo.
Ajib tangu alivyoingia naaonekana
kuitesa vilivyo safu ya mabeki wa JKT
DK 90+4 SIMBA 0-0 JKT
FULL TIME SIMBA 0-0 JKT RUVU
UCHAMBUZI DK 45 ZA AWALI
Simba ambayo
inaongozwa na Joseph Omog kwenye benchi, inaonekana kucheza mpira wa pasi
lakini tatizo ambalo lipo wazi kabisa ni kushindwa kuzitumia nafasi wanazopata
na kingine ambacho ni kikubwa zaidi ni washambuliaji wake kushindwa kutengeneza
njia mbadala ya kuwapita mabeki wa timu pinzani.
Mara nyingi
wanapofika langoni kwa JKT wamekuwa kama hawajui wafanyaje na kujikuta
wakitumia muda mwingi kurudidisha mipira nyuma au wananyang’anywa,
washambuliaji wanatakiwa kuwa na plan B kwani ni kama wameshikwa au
wanagandishwa kila wanapolifikia lango la wapinzani wao. Upande wa mabeki
unaonekana kutulia sana.
JKT RUVU
Inacheza
vizuri lakini wanaonekana kutaka kupiga pasi nyingi zaidi kwa lengo la
kushindana na Simba na hilo linaweza kuwagharimu. Walipata nafasi moja nzuri
ambayo kama wangeitumia ipasavyo basi sasa wangekuwa wana bao moja lakini
kutokana na mpigaji kutokuwa makini katika umaliziaji ulisababisha mpira
uokolewe na mabeki wa Simba.
ILIKUWA HIVI; Mshambuliaji wa JKT alitanguliziwa
mpira na mwenzake ambapo alionekana kuwazidi mabeki wote wa Simba na wakati huo
Angban akawa ametoka kusaidia na kweli akaugusa mpira ambao pia ukarudi kwa
mchezaji mwingine wa Maafande hao ambaye aliutuliza lakini akashindwa kupiga
kiufundi kwani mpira ulitua miguu kwa beki wa Simba ambaye aliuosha mbele, kumbuka
wakati huo Angban alikuwa bado yupo chini.
Post a Comment