MSHAMBULIAJI
wa Yanga, Amiss Tambwe, ameanza kumgwaya Laudit Mavugo wa Simba kutokana na
mpira mwingi aliocheza juzi wakati wakishinda mabao 3-1 dhidi ya Ndanda, katika
mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mavugo
ameonekana kumuibua Tambwe baada ya kusema msimu huu wa Ligi Kuu wanaweza
kufanya vibaya kutokana na uchovu wa kucheza michezo mingi bila kupumzika.
Yanga
wanashiriki hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo wanatarajia
kucheza na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC) katika mchezo wa
marudiano utakaochezwa wiki hii, mjini Lubumbashi.
Akizungumza jana
kabla ya kuondoka, Tambwe alisema msimu wa ligi uliopita wachezaji Yanga
walikuwa na kibarua kigumu cha kutetea taji lao na hawajapumzika, kwani
wameunganisha mechi za kimataifa.
“Uchovu
unaweza kutusumbua, kama utakumbuka tangu tumemaliza ligi tumekuwa katika mashindano
ya kimataifa kwa muda mrefu bila kupumzika, tuna kazi kubwa mbeleni,” alisema
Tambwe.
Tambwe
alisema pamoja na uchovu mkubwa walionao wachezaji wenzake, lakini wamejipanga
vya kutosha kuhakikisha wanatetea ubingwa wao.
Post a Comment