MWANARIADHA wa
Afrika Kusini, Caster Semenya amejishindia dhahabu katika mbio za mita 800
kwenye Michuano ya Olimpiki inayofanyika jijini Rio de Janeiro nchini Brazil.
Franchine
Niyonsaba ameshinda nafasi ya pili na kujishindia medali ya fedha huku Mkenya Margeret
Nyairera Wambui akichukua medali ya shaba.
Semenya
alivunja rekodi ya taifa lake katika mbio hizo na kuweza kushinda kwa dakika
moja dakika 55 na sekunde 28.
Mwanariadha
huyo ambaye alizua utata mwaka 2012 alipofanyiwa ukaguzi wa kijinsia
alijishindia fedha mwaka huo.
''Ndoto ya
mwanariadha yoyote ni kushinda dhahabu hususan katika mbio za Olimpiki,” alisema
Semenya.
Na Marekani
imeshinda mbio za mita 400 mara 4 kupokezana vijiti kwa wanawake na
kujinyakulia nishani ya dhahabu, baada ya kutimka kwa muda wa Sekunde 19.06.
Kina dada
hao wameandikisha ushindi mara sita mtawalia katika mashindano ya Olimpiki.
Kikosi cha
kina dada kutoka Jamaica kilizoa fedha, ilhali Uingereza ikajipatia nishani ya
shaba.
Kikosi cha
wanaume pia cha Marekani kimeshinda mbio za mita mia nne mara nne kupokezana
vijiti.
Naye
mwanariadha wa Uingereza Mohammed Farrah, ameandikisha ushindi mara mbili
katika mbio ndefu za mita elfu kumi na elfu tano mtawalia, huku akizoa dhahabu
baada ya kuwapiku wenzake kwa kasi huko Rio de Janeiro.
Miaka minne
iliyopita alizoa dhahabu mbili katika mbio hizo hizo, katika mashindano ya
Olimpiki Jijini London.
Wakati huo
huo, timu ya soka ya wenyeji Brazil, inafurahia nishani yake ya kwanza ya
dhahabu, katika soka.
Mabingwa hao
mara tano wa Kombe la Dunia waliwanyuka Wajerumani katika mikwaju ya penalti,
baada ya mechi hiyo kumalizikia bao moja kwa moja, hata baada ya kipindi cha
ziada.
Post a Comment