BEKI na nahodha wa zamani wa Arsenal, Tony
Adams amesema hana wasiwasi na hali ya klabu yake kuanza kwa mwendo wa taratibu
katika msimu huu mpya na anaamini matokeo mabaya hayatokani na kutosajili kwa
fedha nyingi.
Adams ambaye ni mkurugenzi wa soka katika moja ya timu inayoshiriki ligi ya China, amesema mashabiki hawatakiwi kuwa na papara ya kutaka kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger atumie fedha nyingi kusajili.
"Kuna wachezaji wengi walikuwa nje,
kupata pointi moja dhidi ya mabingwa, wiki iliyopita yalikuwa ni matokeo
mazuri," alisema Adams na kuendelea:
“Matokeo mabaya katika mechi za kwanza ni
kawaida, bado naunga mkono falsafa za Wenger za kutotumia fedha nyingi kusajili
japokuwa nahisi anatakiwa ‘aibalansi’ timu hasa katika safu ya ulinzi na
ushambuliaji."
Post a Comment