MO KUSHOTO AKIWA NA MKUU WA MKOA WA DAR, PAUL MAKONDA

MFANYABIASHARA anayetaka kununua hisa ndani ya klabu ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, ni kama ameanza kazi kiaina ndani ya Wekundu hao wa Msimbazi baada ya juzi kuwaleta Wazungu wawili waliokuwa wakirekodi mazoezi ya klabu hiyo.

Wazungu hao walikuwa na kamera zao kubwa ambapo walikuwa wakirekodi kila tukio lililokuwa likitokea kwenye mazoezi hayo ambayo yalifanyika Uwanja wa Boko Veterani.

Baada ya mazoezi hayo, Wazungu hao waliwachukua baadhi ya wachezaji na kufanya nao mazungumzo ambapo yote hayo wakati yakitokea walikuwa wakiendelea na shughuli yao ya kurekodi.


Kutokana na hali hiyo, DIMBA lilifanya uchunguzi ili kujua Wazungu hao wana lengo gani ambapo taarifa za chini kwa chini zinadai kuwa ni watu wa Mo ambao wanaanza kufanya mambo kama mpango mkakati wa mfanyabiashara huyo kuiendesha Simba kisasa.

“Unajua huyu jamaa (Mo) ameamua kuiendesha Simba kisasa na hawa Wazungu kuna taarifa wameletwa naye kwani mipango yake ni kuhakikisha kila kitu kinachofanywa na klabu hii kuanzia mazoezi vinakuwa vikirekodiwa.

“Nadhani pia akishakabidhiwa timu ataanzisha TV maalumu ya Simba na ndiyo maana ameanza sasa. Nadhani Wanasimba watafurahi mbele ya safari,” alisema mtu mmoja wa karibu na Mo.

Post a Comment

 
Top