MFANYABIASHARA
anayetaka kununua hisa ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, ameanza
kasi ya kuitumikia klabu hiyo ya Simba kwa kuanza kulipa mishahara ya wachezaji
kuanzia mwezi huu huku suala la kununua hisa likitarajiwa kukamilika ndani ya
mwaka mmoja.
Hatua hiyo
ya Mo imekuja baada ya Kamati ya Utendaji ya Simba kuridhia kubadili mfumo wa
uendeshaji wa klabu kutoka wa sasa wa wanachama na kwenda kwenye mfumo wa hisa,
kufuatia Mo kuhitaji kununua hisa asilimia 51.
Aidha,
kamati itaandaa mkataba wa maridhiano ili kila upande uweze kutekeleza majukumu
yake ambapo Mo alieleza kuwa ataisaidia timu hiyo huku akiwa anaendelea
kusubiria mchakato wa hisa kukamilika.
Mjumbe mmoja
wa Kamati ya Utendaji Simba ambaye aliomba jina lake lifichwe, alisema Mo
ataanza kuwalipa wachezaji mishahara kuanzia mwezi huu.
“Kwa sasa
kuna kamati imepewa kazi ya kuwaelimisha wanachama juu ya suala hilo ili kuweza
kufahamu faida gani watakayoipata juu ya suala hilo ili mwisho wa siku
yafanyike maamuzi sahihi.
“Kwa kuanza,
ataanza na kuwalipa mishahara wachezaji ambapo itaanzia mwezi huu na atapewa
majina ya wachezaji wanaotakiwa kulipwa mishahara ili aweze kuwalipa wachezaji
wote lakini jukumu alilopewa ni juu ya timu tu kwa sasa lakini mambo mengine
yote yatabaki chini ya uongozi.
“Suala lake
nadhani litachukua muda mrefu hata mwaka mmoja hadi kufikia kukamilika kwa
mchakato mzima kufuatia kupata maoni mbalimbali na makubaliano kutoka kwa
wanachama baada ya kupata elimu ya kutosha.
“Hata hivyo
asilimia kubwa ya wanachama hawataki auziwe hisa kubwa ya asilimia 51 na badala
yake auziwe asilimia 48,” alisema bosi huyo.
Alipotafutwa
Msemaji wa Simba, Haji Manara kuzungumzia suala hilo, simu yake iliita bila ya
kupokelewa hata katibu, Patrick Kahemele naye simu yake haikupokelewa.
Tayari Mo
alishatoa msaada wa shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia usajili, kiasi
ambacho Simba ilikitumia kwa ajili ya kukamilisha usajili wa wachezaji kadhaa
nyota walionao hivi sasa.
Post a Comment