Ariana Angel
KOCHA Mkuu wa
Klabu kongwe nchini Misri ya Al Ahly, Martin
Jol amejiuzulu kuifundisha timu hiyo akihofia usalama wake.
Kocha huyo
aliiongoza Al Ahly kuiondosha Yanga kwenye michuano uya Klabu Bingwa Afrika kwa
mabao 3-2 na vijana hao wa Jangwani kuangukia kwenye Kombe la Shirikisho ambako
walitinga hatua ya makundi.
Kocha huyo
ambaye ni raia wa Uholanzi alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja lakini mpaka sasa
ameutumikia kwa miezi sita pekee.
Mashabiki wa
klabu hiyo walionekana kukerwa sana na kushindwa kwa timu hiyo kufika hatua ya
nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika hali ambayo ilionekana kumtisha kocha huyo
wa zamani wa Ajax na Tottenham.
Tangu wakati
huo amepokea vitisho pia kupitia mitandao ya kijamii jambo ambalo anasema
limechangia uamuzi wake wa kuondoka.
Jol
alijibizana na mashabiki Ijumaa iliyopita baada ya timu yake kutoka sare 2-2 dhidi
ya Klabu ya Zesco United na kuzima matumaini yao ya kusonga mbele.
Post a Comment