KOCHA Mkuu wa
Simba, Mcameroon, Joseph Omog, amewapongeza watani wao wa jadi, Yanga, kwa
rekodi nzuri waliyoiweka kwenye Kombe la Shirikisho Afrika huku akiitabiria
makubwa timu hiyo mwakani kwenye michuano hiyo.
Yanga iliondolewa kwenye michuano hiyo katika
hatua ya Nane Bora ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa na pointi nne.
Omog alisema Yanga ilijitahidi kwa hatua hiyo
iliyofikia, hivyo wanastahili pongezi na kikubwa kinachotakiwa kwao ni
kujipanga kwa ajili ya mwakani ili wafike mbali zaidi ya hapo walipofikia mwaka
huu.
Aliongeza
kuwa, ilikuwa ngumu kwa Yanga kusonga mbele zaidi kwenye michuano hiyo kutokana
na kundi kushirikisha timu zenye uzoefu kama TP Mazembe ambayo inashiriki kila
mwaka.
“Mechi yao na
Mazembe, sijajua wamecheza kwa kiwango gani, lakini kikubwa ninawapongeza kwa
rekodi nzuri waliyofikia katika michuano hiyo mikubwa Afrika.
“Ninaamini
mwakani watafika katika hatua nzuri ya michuano kama hiyo baada ya kupata
uzoefu na mbinu zake msimu huu, ilikuwa ngumu kwa Yanga kufika hatua nyingine
kutokana na kundi lao kuwepo baadhi ya timu zenye uzoefu kama Mazembe yenyewe
ambayo kila mwaka inashiriki,” alisema Omog.
Post a Comment