TAYARI
imewekwa wazi mapema kuwa baada ya kukamilika kwa Uwanja wa Uhuru, timu za
Simba na Yanga zitahamia hapo kwa ajili ya mechi zao za nyumbani za Ligi Kuu
Bara, suala hilo halijaifurahisha Simba na limepingwa vikali.
Awali, kabla
ya juzi wajenzi wa uwanja huo kuukabidhi rasmi kwa serikali, tayari Mtendaji
Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura aliweka wazi kuhusiana na azma hiyo ya
kuzihamishia mechi za timu hizo kutoka Uwanja wa Taifa na kuhamia Uwanja wa
Uhuru.
Kocha
Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja ametoa sababu za kuukataa uwanja huo
kuwa utawanyima uhuru wachezaji kuzalisha kile walichojifunza wakiwa mazoezini
na kuwabana katika ufanisi wao wa kazi.
“Uwanja
wenye nyasi bandia kama huo utawanyima wachezaji kuzalisha kile walichokusudia,
kwa maana mazoezi na mbinu wanajifunza kwenye uwanja halisi lakini wakienda
kwenye mechi wanakutana na kitu kingine, hii itawanyima uhuru wa kufanya
ubunifu na mbinu walizonazo.
“Nyasi
halisi kama zile za taifa ni nzuri zaidi na zinaleta uhalisia wa soka, tofauti
na hizi bandia. Nafikiri kama kuna uwezekano wa mtu mwenye uwezo wa kugharamia
gharama za Uwanja wa Taifa, mamlaka iwape tu uwanja huo kwa ajili ya matumizi
lakini vinginevyo Uwanja wa Uhuru hautakuwa mzuri kwa wachezaji,” alisema
Mayanja.
Post a Comment