ARSENAL inatarajiwa kuivaa Leicester
City, leo jioni lakini Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa anaweza
kuamua kuchukua maamuzi magumu ya kuwatumia mastaa wake kadhaa ambao bado
hawapo fiti kucheza mechi.
Arsenal ilianza vibaya mchezo wake wa
kwanza wa Premier League kwa kufungwa dhidi ya Liverpool huku ikiwakosa
wachezaji wake kadhaa ambao walikuwa nje kutokana na kutokuwa fiti kwa kuwa
walipewa mapumziko muda mrefu wa mapumziko.
Wachezaji hao ni mshambuliaji Olivier
Giroud, beki Laurent Koscielny na kiungo mchezeshaji Mesut Ozil ambao tayari
wameshanza mazoezi ya pamoja na wenzao walikuwa kwenye mapumziko baada ya
kumalizika kwa michuano ya Euro 2016 mwezi uliopita.
Wenger anataka kuhakikisha timu yake
inapata ushindi dhidi ya mabingwa wao watetezi ambao nao walipoteza mchezo wao
wa kwanza jambo ambalo linafanya mechi hiyo kuwa ngumu zaidi.
“Nafikiri nitachukua uamuzi ndani ya
saa 40 kutoka sasa (juzi) naweza kufanya mchezo wa kubahatisha wa kuwatumia,”
alisema Wenger na kuongeza:
"Ni mapema mno kutoa uamuzi wa
kuwatumia wachezaji hao ambao hawajacheza kwa muda mrefu. Laurent yeye ana
nafuu na anaonekana kuwa kwenye afya nzuri tofauti na wenzake.
"Michuano ya Euro iliisha Julai
10, kisha ligi inaanza Agosti 14, unategemea nini hapo? lazima mchezaji awe na
muda wa kupumzika.”
Arsenal ilionekana kuyumba katika
nafasi ya beki wa kati katika mchezo uliopita dhidi ya Liverpool na kupoteza
kwa mabao 4-3, inawakosa wachezaji wake wa nafasi hiyo wakiwemo Gabriel na
nahodha wake, Per Mertesacker ambao wote ni majeruhi.
Kuhusu Aaron Ramsey ambaye
anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja, kocha huyo alisema maendeleo yake
bado yanasuasua huku akisema anategemea straika wake, Danny Welbeck anaweza
kurejea wakati wa Krisimasi mwaka huu tofuati na ilivyotegemewa kuwa atarejea
mwakani.
Post a Comment